Ali kiba-Mwana lyrics

Mali ni nyingi nyumbani kipi kimekukimbiza Ona babio mamio wote wanakulilia Mtoto peke yako nyumbani kipi kimekukimbiza Ona babio mamio wote wanakulilia Ndani ya Dar Es Salaama ulikuja bure Tena kimwana kimwana hujui kuchuna Na zile lawama za wale walokuzoeza Ulikuja jana na leo tofauti sana Tena bora yule wa jana wa leo tofauti sana Dakika mbili mbele nyuma kichwa kinauma Tena bora yule wa jana wa jana leo wa jana Dakika mbili mbele nyuma kichwa kinauma oyayee Mbona unawatesa sana? omamee Mbona unajitesa sana? Ukaanza kulewa madawa kuvuta kwa sana ndani ya Dar es Salaam mambo matamu hayakukuisha hamu we bado mtoto kwa mama hujayajua mengi Mwenda tezi na omo marejeo ngamani Amesema sana mama dunia tambara bovu kuna asali na shubiri ujana giza na nuru We mwana wewe mwana, mwana jeuri sana Ulichokifuata hukupata, umekosa ulivyoacha Kwa baba yako mwana na mama yako mwana Kwa vichache ulivyovitaka ni vingi ulivyoacha oyayee Mbona unajitesa sana? omamee Mbona unawatesa sana?
Previous
Next Post »
Thanks for your comment