Ben pol samboira lyrics

(verse 1) asubuhi tu kukicha ,mi nazianza pilika mchana kutwa kutafuta ,nikutunze langu ua na uzuri ulionao ,nakuacha nyumbani peke yako roho inaniuma mwenzio, natamani nishinde kando yako na uzuri ulionao,nakuacha nyumbani peke yako, roho inaniuma mwenzio, natamani nishinde pembeni yako , mi napata homa, njiani na watu ukisimama, na roho inaniuma, sokoni kurudi umechelewa. mi napata homa ,njiani na watu ukisimama, na roho inaniuma , sokoni kurudi umechelewa (chorus) samboira kuruse, sumuka na vyeuye kutaali(kutaali) jichunge mama .. katu sitopenda nikukose mpenzi wee samboira kuruse sumuka ne vyeuye kutaali, jichunge mama katu sitopenda , nikukose mpenzi wee .. (verse 2) ulishajua mi nakujali sana, ndo maana moyo wangu unaniuma , nakuomba kipenzi chunga sana , maana wapo wasiopenda kutuona , ... wakijipitisha kutwa kucha , waambie kwangu umeshafika , usidanganyike na zao pesa , pamba na magari na vya kupita .. (chorus) samboira kuruse ,sumuka ne vyeuye kutaali (kutaaali) jichunge mama katu sitopenda nikukose mpenzi wee ....till fade
Previous
Next Post »
Thanks for your comment